Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando (aliyevaa skafu) akikata utepe kuzindua Kituo cha Rasilimali za Walimu (TRC) kilichofanyiwa maboresho na Vodacom Tanzania Foundation katika Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi, Wilaya ya Ubungo. Uzinduzi wa jengo hilo umeambatana na makabidhiano ya vifaa vya kisasa vya TEHAMA, vikiwemo kompyuta 30 zilizounganishwa na intaneti), UPS 30, meza na viti 30, televisheni ya inchi 75 pamoja na madawati 90 kwa ajili ya wanafunzi. Makabidhiano hayo yamefanywa na Mkuu wa Idara ya Uendelevu na Ubia wa Vodacom Tanzania Foundation, Pauline Koola, huku yakishuhudiwa na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, eneo la Kibaha Fadhili Linga, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi, Lois Bawazir Hassani na mwakilishi wa Afisa Elimu Msingi wilaya ya Ubungo, Hamida Semkuya.
Mkuu wa Idara ya Uendelevu na Ubia wa Vodacom Tanzania Foundation, Pauline Koola, akizungumza wakati wa makabidhiano ya Kituo cha Rasilimali za Walimu (TRC) Mbezi, Ubungo. Kupitia ushirikiano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) katika programu ya MEWAKA, Vodacom Tanzania Foundation imeboresha na kukipatia kituo hicho vifaa vya kisasa, huku ikiwezesha zaidi ya walimu 100,000 kupata mafunzo kupitia mfumo wa LMS bila gharama za data wanapotumia mtandao wa Vodacom, kati ya walimu 300,000 wanaolengwa nchini kote.
Mwonekano wa nje wa jengo la Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi, Wilaya ya Ubungo, baada ya kufanyiwa maboresho na Vodacom Tanzania Foundation. Ukarabati huo umehusisha uwekaji wa dari na viyoyozi, pamoja na upatikanaji wa vifaa mbalimbali vikiwemo kompyuta 30 za mezani zilizounganishwa na intaneti, vifaa vya akiba ya umeme (UPS) 30, seti 30 za meza na viti na televisheni janja ya inchi 75, kwa lengo la kuimarisha mazingira ya walimu kujiendeleza kitaaluma na kutumia teknolojia katika ufundishaji.
Mwonekano wa ndani wa Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi, Wilaya ya Ubungo, baada ya kufanyiwa maboresho na Vodacom Tanzania Foundation. Ukarabati huo umehusisha uwekaji wa dari na viyoyozi, pamoja na upatikanaji wa vifaa mbalimbali vikiwemo kompyuta 30 za mezani zilizounganishwa na intaneti, vifaa vya akiba ya umeme (UPS) 30, seti 30 za meza na viti na televisheni janja ya inchi 75, kwa lengo la kuimarisha mazingira ya walimu kujiendeleza kitaaluma na kutumia teknolojia katika ufundishaji.
Baadhi ya madawati 90 yaliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi, Wilaya ya Ubungo, ikiwa ni sehemu ya mchango wa taasisi hiyo katika kuboresha mazingira ya kujifunzia.
