Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kongani la Viwanda katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba, akiwa ziarani mkoani Mtwara leo tarehe 13 Novemba 2026.

 

PICHA 1-4
Muonekano wa eneo la Mradi wa Kongani la Viwanda katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba, mkoani Mtwara.

PICHA D1-D001

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Viongozi mbalimbali, wakati alipowasili Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba kwaajili ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Kongani la Viwanda, akiwa ziarani mkoani Mtwara, leo tarehe 13 Novemba 2026.

PICHA D2-D0002
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo kuhusu mradi wa Kongani la Viwanda unaojengwa katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba kwaajili ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Kongani la Viwanda, akiwa ziarani mkoani Mtwara, leo tarehe 13 Novemba 2026.

PICHA D4-D0004
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya ubanguaji wa korosho, mara baada ya kuwakabidhi mashine zinazotumia umeme kwaajili ya kubangua korosho, akiwa katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba, akiwa ziarani mkoani Mtwara leo tarehe 13 Novemba 2026.

PICHA D5-D0005
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akibangua korosho kwa kutumia mashine ya umeme mara baada ya kukabidhi mashine hizo kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba, akiwa ziarani mkoani Mtwara leo tarehe 13 Novemba 2026.

 

 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameagiza kufikishwa kwa bomba la gesi na njia maalumu ya umeme katika Kongani ya Viwanda ya Maranje, Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara, ili kuongeza uzalishaji, kuchochea ajira na kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia ubanguaji wa korosho.

Ametoa maagizo hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi na kukagua maendeleo ya kongani hiyo, sambamba na kuzindua mashine 100 za kubangua korosho kwa vikundi vya wajasiriamali, akiwa ziarani mkoani Mtwara.

Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Nishati, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuhakikisha viwanda katika kongani hiyo vinapata nishati ya uhakika ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Amesisitiza kuwa uwekezaji katika umeme unapaswa kuchochea shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato cha wananchi pamoja na kuboreshwa kwa barabara za kuingia katika kongani hiyo ili kurahisisha usafirishaji na shughuli za viwanda.

Kuhusu mashine zilizotolewa kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais ameitaka Bodi ya Korosho Tanzania kuhakikisha wanufaika wanapatiwa mafunzo ya matumizi na utunzaji wake ili uwekezaji huo udumu.

Amesema lengo la kuwawezesha wabanguaji wadogo kuongeza thamani ya korosho halitafikiwa iwapo mashine hizo zitaharibika na kuwalazimisha kurejea katika matumizi makubwa ya mikono. Kwa maelezo yaliyotolewa katika hafla hiyo, kila mashine imegharimu zaidi ya shilingi milioni sita.

Akizungumzia maendeleo ya kongani hiyo, Makamu wa Rais amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa na kuahidi kuwa Serikali Kuu itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Mtwara kuimarisha miundombinu na mazingira ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema kila moja ya mashine 100 zilizozinduliwa ina uwezo wa kubangua kilo 700 za korosho kwa siku, hivyo kufikisha uwezo wa pamoja wa tani 70 kwa siku. Mpango huo unalenga kutoa ajira kwa vijana wasiopungua 4,000 kwa mwaka. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred, amesema kongani hiyo ni sehemu ya jitihada za kuongeza ubanguaji nchini badala ya kuuza korosho nje zikiwa ghafi, huku lengo likiwa korosho zote zinazozalishwa nchini zibanguliwe na viwanda vya ndani ifikapo mwaka 2030.

Ameeleza kuwa eneo la kongani lina ukubwa wa ekari 1,500, ambapo ekari 350 zinatumika kwa sasa. Tayari wawekezaji tisa wako tayari kuwekeza, huku miundombinu ya awali ikiwa imekamilika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota, amesema kuongezeka kwa shughuli za ubanguaji kumeanza kuchochea ushindani katika soko la korosho. Hata hivyo, ameomba wakulima wapatiwe pembejeo za kutosha na kwa wakati ili kuongeza uzalishaji. Amesema upanuzi wa mashamba unahitaji kuendana na ongezeko la pembejeo ili wakulima wanufaike na mahitaji ya malighafi katika viwanda.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo ameeleza kuwa kulikuwa na upungufu wa salfa ya unga katika msimu uliopita na kwamba tathmini inaendelea kubaini sababu za uzalishaji kuwa chini ya matarajio. Wizara imeahidi kufanyia kazi maombi ya kuongeza pembejeo na kuhakikisha zinawafikia wakulima mapema.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameahidi kupeleka shilingi bilioni nne kabla ya mwisho wa mwezi Novemba ili kuendeleza mradi wa Makonde, pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi mingine ya maji inayotekelezwa mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais yuko katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Mtwara, kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.