Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akizungumzia kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalmbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalimbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalimbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Salum Ramadhan akizungumza katika Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akizungumzia kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalmbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Mwanajuma Juma akiuliza Maswali katika Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akizungumzia kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalmbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Mwandishi wa Habari wa Faya Bez Redio Yahya Saleh Furaha akiuliza Maswali katika Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zahor Matar Masoud akizungumzia kuhusiana na Mikutano ya Wizara mbalmbali za Serikali na Waandishi wa Habari ambapo itafanyika kila baada ya Miezi Miwili na kutoa Bei Elekezi za Viwanja vya Michezo Vilivyojengwa katika Mikoa na Wilaya ,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

……………. 

Na Maelezo Zanzibar 12.11.2026

WIZARA ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar imeweka utaratibu wa matumizi na bei elekezi za viwanja 17 vya michezo vilivyojengwa katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo na kuondoa mkanganyiko wa gharama za matumizi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Migombani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mattar Zahor Masoud, amesema viwanja hivyo vimejengwa kwa lengo la kuongeza fursa kwa vijana kushiriki shughuli za michezo katika mazingira bora na yenye huduma muhimu.

Amesema utaratibu huo umeandaliwa ili kuhakikisha wananchi, vilabu na timu mbalimbali zinapata fursa ya kutumia viwanja hivyo kwa gharama zinazoeleweka kwa mfumo madhubuti wa kuviendesha na kuvitunza.

Ameeleza kuwa viwanja hivyo 17 vimeongezwa katika idadi ya viwanja vilivyokuwepo awali, ambapo Wizara imeamua kuviendesha kwa utaratibu wa ubia na wawekezaji ili kuhakikisha vinaendelea kutoa huduma kulingana na male [email protected] ngo yaliyokusudiwa.

Amesema kuwa viwanja hivyo vimegawanywa katika madaraja matatu, ambapo daraja la kwanza linahusisha viwanja vyenye mabweni na huduma nyingine muhimu, vikiwemo kiwanja cha Pangatupu kwa Unguja na Kinyikani kwa Pemba.

Amesema daraja la pili linahusisha viwanja vitatu ambavyo ni Matemwe na Kutogani kwa Unguja pamoja na Kangani kwa Pemba, huku daraja la tatu likiwa na viwanja tisa vilivyosambazwa katika wilaya mbalimbali za Unguja na Pemba, isipokuwa Wilaya ya Magharibi A.

“Baadhi ya viwanja hivyo tayari vimeanza kutumika, lakini Wizara imekuwa ikipokea malalamiko kuhusu gharama za matumizi hivyo tumeona ni bora kuweka viwango rasmi ili wananchi wafahamu kiasi kinachotakiwa kulipwa” ameeleza.

Akifafanua viwango vya malipo kwa Uwanja wa Mao Zedong, ambao umekabidhiwa na Halmashauri ya Jiji, amesema mechi za kirafiki zitakazofanyika Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia asubuhi hadi jioni na kutozwa shilingi 150,000, huku matumizi ya usiku yakigharimu shilingi 200,000 kwa kila mechi.

Amesema michezo ya taasisi zitatozwa shilingi milioni 1.2 kwa matumizi ya mchana na shilingi milioni 1.5 kwa matumizi ya usiku, wakati matamasha yatakayofanyika kuanzia asubuhi hadi usiku yatagharimu shilingi milioni 2.5 na shughuli za mahafali shilingi milioni tano.

Amefafanua kuwa mashindano yanayoandaliwa na Wizara yatakuwa bure, huku yale yanayoandaliwa na wadau wengine yatatozwa shilingi 100,000 ambapo ligi za mpira wa miguu za Ligi Kuu, Kanda na Mkoa zitachangia asilimia 20 ya makusanyo.

Amefafanua kuuhusu matumizi ya viwanja kwa ajili ya mazoezi, amesema vilabu vitakavyotumia viwanja hivyo kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 5:30 vitatozwa shilingi 500,000 kwa mwezi, huku akademi zikitozwa shilingi 100,000 kwa mwezi.

Amesema vilabu vitakavyofanya mazoezi ya mchana katika michezo ya ndani vitatumia viwanja hivyo bila malipo, lakini kwa mazoezi ya usiku vitachangia shilingi 30,000 kwa ajili ya huduma ya taa.

Aidha amebainisha kuwa ukumbi uliopo katika Uwanja wa Mao Zedong kwa matumizi ya kawaida yatatozwa shilingi 20,000 kwa mchana na shilingi 50,000 kwa usiku, huku mikutano na mafunzo yakitozwa shilingi 500,000.

Aidha, amesema ligi za wilaya za daraja la kwanza zitapata fursa ya kutumia uwanja bure kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00, wakati ligi za wilaya za daraja la pili na la tatu zitatozwa shilingi 30,000 kuanzia saa 6:00 mchana.

Ameongeza kuwa programu za mafunzo kwa waamuzi zitakuwa bure sambamba na mazoezi ya waamuzi katika viwanja vya wilaya ambayo pia yatafanyika bila malipo.

Katika hatua nyingine, amesema matumizi ya viwanja kwa shughuli za elimu yatatozwa shilingi 500,000 huku vyuo vikuu vikitozwa shilingi milioni moja.

Amesema Wizara inatarajia utaratibu huo utasaidia kupunguza gharama na kuweka uwazi katika matumizi ya viwanja hivyo na kuhakikisha vinatunzwa na kuendelea kutoa huduma kwa vijana na wananchi kwa ujumla.

Amebainisha kuwa jumla ya dola za Marekani milioni 54 zimetumika katika ujenzi wa viwanja hivyo, hivyo ni muhimu kuwepo kwa mfumo mzuri wa uendeshaji na utunzaji ili viendelee kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.