Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog,Dodoma

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limetangaza nafasi za kujiunga na Mafunzo ya Jeshi kwa kujitolea kwa mwaka 2026/27 kwa Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani.Akitangaza nafasi hizo mbele ya vyombo vya habari  Novemba 12,2026 makao makuu ya JKT Jijini Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema utaratibu wa Vijana hao kuomba na hatimaye kuchaguliwa unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi. 

“Vijana wenye taaluma mbalimbali zikiwemo `Diploma in Information Technology”, `Diploma in Business Information Systems”, `Diploma in Computer Science”, “Diploma in Information and Communication technology (ICT)”, “Diploma in Cyber Security and Digital Forensics”, “Bachelor of Science in Computer Science”, “Bachelor of Science in Information Technology”, “Bachelor of Science in Computer ngineering”, “Bachelor of Science in Business Information Technology”, “Bachelor of Science in Cyber Security and Digital Forensics”, `Bachelor of Science in Computer Networks and information Security Engineering” na Walimu wa VET kwenye fani za uchomeleaji, Ufundi Magari, Umeme wa Magari, Ufundi Bomba, Ufundi Rangi, Uashi, TEHEMA, Ubunifu wa mavazi, ukarani, useremala, ushonaji, ufundi friji na viyoyozi, wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao,”amesema.

Amesema usaili wa Vijana hao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 16 Novemba 2026 kwa Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya JKT kuanzia tarehe 10 Desemba 2026 hadi 15 Desemba 2026.

Pia amewakumbusha Vijana hao watakaopata fursa kuwa JKT haitoi ajira na haihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali, bali hutoa Mafunzo yatakayosaidia kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza Mkataba wao.

“Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika Tovuti ya JKT ambayo ni www.ikt.mil.tz ,”amesema.