Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania Tulisindo Mlupilo (kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank Ndabu Lilian Swere, (katikati) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited Rwebu Mutahaba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo imezinduliwa kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited, kwa lengo la kuimarisha uwazi, kurahisisha usimamizi wa michango na kuhakikisha wanachama wanapata taarifa za miamala ya vikundi vyao.

[11/10, 8:35 PM] Tipher Hesa: Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa M-PESA MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 10, 2026, jijini Dar es Salaam, kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited.Meneja wa Huduma Mpya za Kifedha wa M-Pesa, Brenda Msola akielezea namna huduma mpya ya kidijitali ya M-PESA MCHEZO, inayowawezesha Watanzania kuanzisha na kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa, inavyofanya kazi. Wateja wanaweza kujiunga kwa kupiga *150*00#, kuchagua Huduma za Kifedha kisha M-PESA MCHEZO na kuanzisha au kujiunga na vikundi, kuchangia fedha na kufuatilia michango pamoja na taarifa za miamala.

Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank, Ndabu Lilian Swere (wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited, Rwebu Mutahaba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka kampuni hizo wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 10, 2026, kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc pamoja na watengenezaji wa maudhui, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa, Tulisindo Mlupilo, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kuanzisha na kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo inawawezesha wanachama kuanzisha au kujiunga na vikundi, kuchangia fedha na kufuatilia michango pamoja na taarifa za miamala ya vikundi vyao.