Na MWANDISHI WETU
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imewataka watanzania kuendelea kuwa na imani nayo na kwamba imejipanga kikamilifu kuwapa ushirikiano.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Omar Ali Bhai , alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Mwenyekiti wa tume hiyo, Dunford George Mpelumbe cha kuzungumza na wafanyakazi wa THBUB Tawi la Dar es Salaam.

Bhaia amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, anawahakikishia watanzania kuwa na imani nayo kwa kufikisha changamoto na kwamba itazifanyia kazi.

Wengine wanachangamoto lakini za malalamiko lakini sasa hivi mambo yameendelea. Mtu anaweza kutuma changamoto zake kwa njia ya kidigitali na atahudumiwa.

“Kama mlivyo sikia katika uapisho wetu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuagiza maagizo muhimu tusisubiri malalamiko. Sisi kama tume tumejipanga kwa dhati na kama mnavyoona ni vijana tutahakikisha tunaweza kufikia malengo ya tume,”amesema Bhai.
Ameeleza pia zipo njia nyingi za watanzania kuifikia tume hiyo ikiwa ni pamoja na mfumo wa kidijitali na mashauri yote yanayowasilishwa yanafanyiwa kazi.

“Ninawaomba wananchi wazidishe imani na tutaenbdelea kushirikiana na wananchi wote na naviomba vyombo vya habari wakiwa wadau kutoa taarifa mbalimbali kushirikiana kufafanikisha malengo ya tume,”ameeleza Bhai.

Awali Katibu Mtendaji wa THBUB Tawi la Dar es Salaam, Patience Ntwina, ameeleza wamejipanga kikamilifu kuhakikisha utendaji kazi unasonga mbele ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali.

Naye Ofisa Mfawidhi i wa THBUB Tawi la Dar es Salaam, Shoma Philip, amesema tawi hilo limeendelea vizuri na utendaji wa majukumu.

“Kwa mujibu wa taarifa ya Oktoba 2026, udadi ya malalamiko ya nyuma ya Haki za Binadamu yalikuwa 26, Utawala Bora 103 na Haki Jinai ni 127 hivyo jumla ya malalamiko ni 256,”amesema Shoma.
Ameeleza idadi ya malamiko mapya yaliyopokelewa ya Haki za Binadamu mawili, Utawala Bora moja na Haki Jinai matatu hivyo kufanya jumla kuwa sita.

Kwa upande wa idadi ya malalamiko yaliyofungwa/ yaliyoombewa vibali vya kufunga zamani yaliyo husu Haki za Binadamu mawili, Utawala Bora manne, Haki Jinai matano na jumla yalikuwa 11.
Shoma amesema hakukuwa na malalamiko mapya yaliyofungwa au kuombewa vibali vya kufunga.

“Jumla ya malalamiko yanayoendelea kushughulikiwa yanayohusu Haki za Binadamu ni 28, yanayohusu Utawala Bora ni 104 na yanayohusu Haki Jinai ni 130 hivyo jumla ni 262,” ameeleza Shoma.

Hivi karibuni Rais Dk. Samia, alimteua Dunford George Mpelumbe, kuwa Mwenyekiti wa THBUB na Omar kuwa Makamu Mwenyekiti ambapo viongozi hao wameaipishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam,jana na baada ya kuapishwa walifika katika Ofisi za tume hiyo Tawi la Dar es Salaam, kujitambulisha na kuzungumza na wafanyakazi wa tawi hilo.