Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa Katavi imekutana na kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Katavi, kamati hiyo imekutana tarehe 9 Novemba, 2026 Mjini Mpanda
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa wa Katavi, ambaye pia ni Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Bi. Jospehine Chilongozi* ameongoza kikao hicho, ambacho pamoja na masuala mengine kilisikiliza mgogoro wa ardhi kati ya Wananchi wa Kijiji cha Keshelami na Wavamizi unaohusisha eneo la ekari 3500 uliodumu kwa miaka 7.
Aidha, Kamati hiyo pia imejadili juu ya mpango wa utekelezaji wa majukumu ya kamati pamoja namna ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria kwa wananchi.

