Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaondoka nchini leo tarehe 10 Novemba, 2026 kuelekea jijini Antalya, Uturuki, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Akiwa Antalya, Rais Dkt. Samia atahutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (Antalya Leaders’ Summit), pamoja na kushiriki kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika (High-Level Event on Clean Cooking in Africa).
Aidha, Rais Dkt. Samia atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.
Mkutano wa COP31 unaendelea nchini Uturuki, ukiwaleta pamoja nchi wanachama kujadili hatua za kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
