Mkutano huu unafanyika kwa Ngazi tatu. Ngazi ya wataalamu tarehe 9 hadi 11, Ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 12 na hatimae Ngazi ya Mawaziri tarehe 13 Novemba 2026,

Katika Ngazi ya wataalamu, ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na Bw. Benjamini Mwesiga, Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji (DTIPS) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Ujumbe huo unajumuisha pia wawakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani (FCC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Miongoni mwa maswala yatakayo jadiliwa ni taarifa za kamati ya forodha; kamati ya biashara; pamoja na taarifa kuhusu masuala ya ushindani. Mkutano huo pia utajadili mawasilisho ya nchi Wanachama kuhusu maswala mbali mbali.

Majadiliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wanachama na kupanua fursa za biashara na uwekezaji katika Jumuiya.