MSIMAMIZI wa PTACC Africa, Dkt. Yvonne Olando akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha


………..
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kuvunja mkataba na fundi anayejenga majengo ya huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Same ifikapo Novemba 15, 2026, endapo hatakuwa amekamilisha ujenzi huo.
Agizo hilo limetolewa baada ya kubainika kwa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo kuchelewa kwa ujenzi, uwezo mdogo wa kifedha wa fundi, ujenzi usiozingatia viwango pamoja na kutokuwepo kwake mara kwa mara eneo la mradi.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Kasilda pia ameitaka Halmashauri kufanya uchunguzi kuhusu usimamizi hafifu wa miradi unaofanywa na wahandisi, hali inayosababisha kasoro na kurudiwa kwa baadhi ya kazi.
Amesema awamu ya tatu ya mradi huo ina thamani ya Sh milioni 800, huku Serikali ikiwa tayari imetoa zaidi ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kuanza awamu ya nne tangu Januari 2026.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Jimson Mhagama, amesema amepokea maelekezo hayo, huku TAKUKURU ikiahidi kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Same unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh bilioni saba, ambapo hadi sasa Serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni tano.
