Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 28, 2026, amewasili Moscow, nchini Urusi, ambapo anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi unaofanyika kuanzia leo Oktoba 28 hadi 29, 2026.
Mkutano huo utakaowakutanisha viongozi wa Urusi na nchi za Afrika na utaongozwa kwa pamoja na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Fredrick Ibrahim Kibuta, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Domodedovo, Moscow nchini Urusi.

