Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, akizungumza na mafundi walioshiriki ujenzi wa nyumba mpya za makazi katika Chuo cha Magereza Kiwira, jijini Mbeya, baada ya kuzindua nyumba hizo, wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Awali ya Askari Wanafunzi wa Jeshi la Magereza, Kozi Na. 33, Oktoba 17, 2026.