……………………………………………………………………..
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amekabidhi vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Covid 19 vinavyosababishwa na virusi Corona.
DC Waryuba amemkabidhi Mganga Mkuu wa wilaya Tandahimba Dk. Antipass Swai vifaa vyenye thamani ya Tsh. Milioni sitini na mbili laki sita na elfu arobaini (62,640,000/=) ambapo amewasihi Wataalamu hao wa afya kuvitunza vifaa hivyo na viwaongezee kasi ya mapambano ya virusi vya Corona na kuisihi jamii kutiana moyo na kuacha kupeana hofu na kuungana kwa pamoja kupambana na adui Covid 19.
“Wakati huu ni wa kutiana moyo na kuungana kwa pamoja kumshambulia adui Corona. Vifaa hivi viende kuongeza matumaini na kasi kubwa ya mapambano na ushindi. Nawasihi Wataalamu vitunzeni vifaa hivi.” Alisisitiza DC Waryuba.
DC Waryuba aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya amekabidhi Mashine mbili za kupumulia, barakoa, PPE, mabuti, ndoo pamoja na Majaba.