……………………………………………………………………………………………..
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wamekabidhi jengo la makazi ya watumishi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) lililopo katika Makao Makuu ya Shamba la Miti Sao Hill – Mafinga.
Jengo hili limejengwa kwaajili ya makazi ya watumishi wa TFS – Shamba la Miti Sao Hill ambalo litatumika kwa makazi ya familia mbili za watumishi (semi detarch). Akizungumza wakati wa kukabidhi jengo hilo Meneja wa NHC Mkoa wa Iringa Bw. Repson Yosiah amesema kuwa wamekamilisha jengo hili kwa wakati ili litumike kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Naye Mwakilishi kutoka TFS Mhandisi Kaston H. Sanga amewashukuru NHC kwa kukamilisha jingo hili kwa wakati na hivyo linaenda kusaidia watumishi waliopo katika Shamba la Miti Sao Hill ikiwa ni sehemu ya mikakati ya TFS.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bw Juma Mwita Mseti amesema kuwa anaishukuru TFS kwa kuendelea kuona umuhimu wa kujenga makazi ya watumishi kwani inasaidia kuboresha utendaji wa kazi ikiwa watumishi wote kukaa karibu na eneo wanalolifanyia kazi.
Jengo hili limejengwa na TFS kupitia NHC kwa gharama ya Tsh 229,369,589 ikiwa ni sehemu ya mikakati ya taasisi ili kuboresha miundo mbinu ambayo husaidia katika utendaji wa kazi wa kila siku ili kuongeza ufanisi na hivyo kufikia malengo ya taasisi.
#misitukwanza