Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mh. Shaka Hamdu Shaka, amepongeza hatua na uamuzi wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kujenga upya Daraja la Magole, katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma.
Akizungumza leo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mh. Masanja Kadogosa, DC Shaka amesema daraja hilo ni nyezo muhimu ya uchumi wa Taifa, na ujenzi wake ni matumaini mapya kwa Watanzania katika kuimarisha miundombinu ya madaraja na barabara zitakazopitika wakati wote.

