Mkuu wa Kitengo cha Kliniki ya Bima, Wagonjwa Maalumu na Wagonjwa kutoka Nje ya Nchi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Caroline Swai, akizungumza na wageni kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires ya nchini Algeria walipotembelea ORCI kwa lengo la kujionea huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa na taasisi hiyo pamoja na kujadili fursa za ushirikiano zitakazochangia kuboresha huduma za matibabu ya saratani.Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Nanzoke Mvungi akimkabidhi zawadi Mgeni kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires iliyopo Algeria, wakati yeye na wenzake walipotembelea ORCI kwa lengo la kuona huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa pamoja na kujadili fursa za ushirikiano utakaosaidia kuboresha huduma za matibabu ya saratani.

Mkuu wa Kitengo cha Famasi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Zawadi Phares akimkabidhi zawadi Amine Dembri ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba na Mikakati ya Masoko wa kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires kutoka Algeria wakati yeye na wenzake walipotembelea ORCI kujionea huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa na kujadili fursa za ushirikiano kwa ajili ya kuboresha huduma hizo.Mfamasia kutoka Wizara ya Afya Sylvester Maige akimkabidhi zawadi Nihel Younsi ambaye ni Meneja wa Uendeshaji wa Mauzo ya Nje wa kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires kutoka Algeria wakati yeye na wenzake walipotembelea ORCI kwa lengo la kuona huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa pamoja na kujadili fursa za ushirikiano utakaosaidia kuboresha huduma za matibabu ya saratani.

Wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) na Kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires kutoka nchini Algeria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya wataalamu kutoka nchini humo kumaliza ziara yao ya kutembelea ORCI kwa lengo la kuona huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa pamoja na kujadili fursa za ushirikiano utakaosaidia kuboresha huduma za matibabu ya saratani.

Mkuu wa Kitengo cha Famasi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Zawadi Phares akizungumza na Amine Dembri ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba na Mikakati ya Masoko wa kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires kutoka Algeria wakati yeye na wenzake walipotembelea ORCI kujionea huduma za kibingwa za matibabu ya saratani zinazotolewa na kujadili fursa za ushirikiano kwa ajili ya kuboresha huduma hizo.

………….. 

Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam

09/10/2026 Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) imekutana na ujumbe kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Les Laboratoires ya nchini Algeria kujadili fursa za ushirikiano katika upatikanaji wa dawa za saratani kwa lengo la kuimarisha huduma za matibabu kwa wagonjwa.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha mahusiano kati ya ORCI na kampuni hiyo pamoja na kutafuta fursa za ushirikiano zinazoweza kusaidia upatikanaji wa dawa zinazohitajika katika matibabu ya saratani na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wagonjwa.

Akizungumza na wageni hao jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Kliniki ya Bima, Wagonjwa Maalumu na Wagonjwa kutoka Nje ya Nchi wa ORCI, Dkt. Caroline Swai alisema kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta ya afya ni muhimu katika kutafuta fursa zinazoweza kusaidia kuboresha upatikanaji wa mahitaji muhimu kwa ajili ya matibabu ya saratani na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Dkt. Caroline alisema ORCI inaendelea kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa wagonjwa wanaohitaji uchunguzi na matibabu ya saratani, ikiwa ni sehemu ya jukumu la taasisi hiyo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma zinazokidhi mahitaji yao ya kiafya.

Alieleza kuwa ORCI inaendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa kuzingatia umuhimu wa uchunguzi sahihi, matibabu yanayofaa na ustawi wa wagonjwa katika hatua mbalimbali za matibabu yao.

“Huduma hizi ni sehemu ya juhudi za ORCI za kuhakikisha wagonjwa wa saratani wanapata huduma bora zinazozingatia mahitaji yao ya kiafya. Tunaendelea kutoa huduma za kibingwa zinazolenga kuboresha hali za wagonjwa na kuwasaidia kupata huduma wanazohitaji katika safari yao ya matibabu,” alisema Dkt. Caroline.

Kwa upande wake, Amine Dembri Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba na Mikakati ya Masoko wa kampuni ya Les Laboratoires kutoka Algeria, alisema ziara hiyo imewapa fursa ya kufahamu huduma za kibingwa zinazotolewa na ORCI na kujadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya matibabu ya saratani.

“Tumepata fursa ya kujadili maeneo ya ushirikiano yanayoweza kuimarisha utoaji wa huduma za matibabu ya saratani na kuongeza mchango wa wadau katika kuboresha huduma za afya,”.

“Ushirikiano katika upatikanaji wa dawa za saratani ni eneo muhimu linaloweza kuchangia juhudi za kuboresha huduma za matibabu, kwa kuzingatia mahitaji ya wagonjwa na umuhimu wa upatikanaji wa dawa zinazohitajika katika mchakato wa matibabu,” alisema Dembri.

ORCI inaendelea kuimarisha mahusiano na wadau wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutafuta fursa za ushirikiano zitakazochangia kuboresha huduma za saratani na kuongeza manufaa kwa wagonjwa wanaohudumiwa na taasisi hiyo.