Afisa miradi ya jamii wa Vodacom Tanzania Foundation, Deborah Kaluzi (kulia) akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Makumbusho, Yasini Shehaghilo (kushoto). Hafla hiyo ni sehemu ya mpango wa kusaidia shule mbalimbali unaotekelezwa kupitia msafara wa Nyerere Cycling Tour 2026.
Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Archie James Killo (wa pili kushoto) na Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa (wa pili kulia).
Mpango huo unaakisi dhamira ya uboreshaji miundombinu ya elimu na kusaidia jamii zilizopo kando ya njia ya safari hiyo kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa, ugawaji wa madawati pamoja na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ya jamii.
Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour Gabriel Landa (kushoto), akiwa pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakipanda mti ikiwa ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation za kurekebisha mazingira. Kupitia Nyerere Cycling Tour 2026, Vodacom inaunga mkono mipango ya upandaji miti kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Afisa miradi wa Vodacom Tanzania Foundation Deborah Kaluzi, akizungumza na wanafunzi na wadau wa elimu katika Shule ya Msingi Makumbusho, mojawapo ya shule zinazoungwa mkono na Nyerere Cycling Tour 2026, baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation za kuimarisha upatikanaji wa elimu bora, kusaidia shule kuwa na vifaa muhimu vya kujifunzia na kuchangia maendeleo endelevu ya jamii.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makumbusho wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waendesha baiskeli baada ya kukabidhiwa madawati yaliyotolewa kupitia Nyerere Cycling Tour 2026. Mpango huu unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia ikiwa ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation katika kusaidia sekta ya elimu, kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa muhimu vya kujifunzia na kuchangia maendeleo ya jamii kupitia uwekezaji katika elimu bora kwa watoto.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Makumbusho Yasini Shehaghilo (kushoto), Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya kaskazini, Andrew Temu(wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Archie James Killo (wa tatu kutoka kushoto), na Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa (kulia), wakishiriki zoezi la upandaji mti katika Shule ya Msingi Makumbusho. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation kupitia Nyerere Cycling Tour 2026 za kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kuongeza uoto wa asili na kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya jamii na vizazi vijavyo.
