*************************************
Na Woinde Shizza , KILIMANJARO
Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa Ya Moshi Juma Raibu Juzi Amekabidhi barakoa 100 na sanitizer pamoja na Ndoo Kwa wafanyabiashara wa Soko la pasua ili kujikinga na Virus vya Corona ambavyo vinaendelea kutikisa dunia.
Akiongea wakati akikabidhi vifaa hivyo Diwani huyo alibainisha kuwa ameamua kutoa vifaa vya kujikinga na ugonjwa Corona kwa wananchi hao ,ili viweze kuendelea kuchukuwa taathari
Alisema kuwa mbali na kutoa vifaa hivyo pia ameweza kugawa elimu ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona 19 kwa wananchi wa kata ya Bomambuzi pamoja na wafanyabiashara wa masokoni ya pasua pamoja mbuyuni huku alibainisha kuwa wataendelea kutoa vifaa vyakujikinga na elimu kwa kila mwananchi.
Aidha aliwaasa Wananchi hao kufata Maelekezo ya Wataalamu wa Afya na Maagizo Ya Serikali huku wakizingatia zaidi Kuepuka Misongamano Isiyo Ya Lazima.
Pia Diwani huyo aliwaonya wananchi wanaopotosha jamii kuhusu idadi ya wagonjwa pamoja na wanafariki kwa virusi vya Corona na kusema kuwa iwapo atabainika mtu anafanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa thidi yake, huku akiliagiza jeshi polisi kuwachukulia hatua kali za kisheriavifaa hivyo .
alisema wamehamasisha jamii juu ya kuweka na kunawa na maji tiririka na sabuni kwenye sehemu zote za biashara nyumbani na maeneo yote yenye mikusanyiko, wametoa elimu kwenye masoko.
Alishukuru kwa msaada huo mmoja was wafanya biashara wa soko la Pasua Gloria Mboya alisema kuwa anashukuru kwa diwani huyo kwa kuendelea kuwajali wananchi wake kwa kuwapa vifaa vya kujikinga pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kuendelea kuchukuwa tahathari ya ugonjwa huo.
Alisema kuwa ugonjwa huo upo hivyo ni vyema kila mtanzania kuendelea kujikinga na kufuata maelezo yanayotolewa na wataalam,huku akikisitiza kuwa iwapo mtu yeyote akijihisi anadalili za ugonjwa huo kuwa maramoja hospital kwa ajili ya kupata huduma.
Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa Ya Moshi Juma Raibu akiendelea kuwafundisha wananchi namna ya kuvaa barakoa(picha na Woinde Shizza, Kilimanjaro)