*******************************
Viongozi wa UVCCM Kata 18 za Wilaya ya Nyamagana, leo Jumatatu wamepatiwa Lita 180 za sabuni na Katibu wa UVCCM Wilaya ndugu Malanyingi Matukuta ambazo walipatiwa na UVCCM Mkoa wa Mwanza.
Zoezi hili la kugawa sabuni lilianza tarehe 20 April na kuongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza comrade Jonas Lufungulo na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza comrade Dennis Luhende.
Katibu Matukuta ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ndugu Shaban Abdallah ambaye ni mjumbe wa kamti ya utekelezaji wilaya, amekabidhi lita 10 kwa Katibu na mwakilishi wa Kata zote 18 na kuwataka viongozi hao wakaweke kwenye vifungashio na kugawa kwenye maeneo ambayo yanauhitaji na muhimu pia kuwataka kuendelea kutoa elimu juu ya maambukizi ya ugonjwa wa corona kwa wananchi na makundi ya wafanyabiashara ndani ya kata zao kama sehemu ya kutekeleza agizo la Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally aliyetaka Jumuiya ya Vijana kusimamia suala la kuelimisha jamii na kufanya tathimini ya kutosha kama wananchi wamepata elimu inayotolewa na wataalam wa afya katika kuepuka na kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.