Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ( ICC) imepata Tanzania nafasi ya elimu kwa mwanasheria ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupewa nafasi hiyo .

Mtanzania aliyepewa nafasi na Mahakama hiyo ni Revocatus Kuuli ambaye amewasili The Hague juzi katika mafunzo hayo ya siku zisizopungua 10.

Mafunzo hayo yanayoendelea katika moja ya ukumbi wa makao makuu ya ofisi hizo yanalenga kuwajengea uwezo wa sheria kutoka Nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika huku Tanzania ikiwa mojawapo .

Kuuli amesema anashukuru kupata nafasi hiyo adhimu na anaamini itazidi kumjengea uwezo katika shughuli zake zakisheria huku akiishukuru Serikali ya Tanzania .

Kuuli aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka NchininTff .

Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Igunga kabla hajazama zaidi katika masomo yake ya kisheria .