……..
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa amesema uwepo wa Kiwanda cha Chumvi cha STAMICO kilichopo Lingaula, Wilaya ya Kilwa ni fursa ya kipekee kwa wakulima na wazalishaji wa chumvi mkoani Lindi kujifunza teknolojia ya uongezaji thamani na kuwekeza zaidi katika sekta ya chumvi.
Mhe. Dkt Kiruswa ameyasema hayo leo katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji (Lindi Mining Expo 2026) yanayoendelea Wilayani Ruangwa, baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Mwandamizi wa STAMICO, Bw. Mark Mahungo wakati alipotembelea Banda la STAMICO.
Akimkaribisha katika banda la STAMICO, Bw. Mahungo alimuelezea Mhe. Dkt Kiruswa tayari kiwanda kimeanza uzalishaji na
Chumvi inayosafishwa na Kiwanda hiki ni Safi, Salama na yenye Virutubisho asilia, ambayo imekidhi viwango vyote vya ubora vya Kimataifa.
Mahungo ametumia fursa hiyo kuwaalika wananchi wote wa Lindi kuja kujionea Kiwanda hiki na kujifunza zaidi kuhusiana na chumvi inayoandaliwa na kuongezewa thamani.
Maonesho ya Madini Ruangwa yanayobeba kaulimbiu isemayo “Madini na Teknolojia, Fursa ya Uchumi Lindi” yamefungwa rasmi leo na Mhe. Dkt Kiruwa Naibu Waziri Madini, huku akiagiza kuanza mapema kwa maandalizi ya maonesho yajayo.

