Geneva: 15 Septemba, 2026
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), na Makamu wa Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a alikutana na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization – WMO) Prof. Celeste Saulo na kufanya mazungumzo kuhusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa, hali ya El Nino 2026 na umuhimu wa kuendelea kuimarisha utoaji wa taarifa za mapema na maandalizi ya kukabiliana na athari zake.
Prof. Saulo alimpongeza Dkt. Chang’a na kufurahishwa na namna TMA wanavyoendelea kusimamia vyema utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini Tanzania hususan katika kutoa elimu na kutahadharisha Umma na Wadau mbalimbali kuhusiana na hali ya El Nino na athari zake katika misimu ya mvua. Aidha, Prof. Saulo ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za hali ya hewa kupitia programu mbalimbali za WMO ikiwa ni pamoja na eneo la matumizi ya akiliunde (AI) katika mnyororo mzima wa utoaji wa huduma za hali ya hewa.
“Napongeza juhudi za Tanzania katika utoaji wa huduma za hali ya hewa na elimu hususan katika kipindi hiki tunachokabiliwa na Hali ya El Nino yenye nguvu. Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa na nimetumia Tanzania kama mfano mzuri wa utoaji wa elimu kuhusu El Nino na maandalizi ya kukabiliana na hali hiyo katika hotuba yangu ya hivi karibuni kuhusiana na hali inavyoendelea” Alisema Prof. Celeste Saulo.
Katika Kikao hicho, Dkt.Chang’a alimshukuru Katibu Mkuu wa WMO kwa kuendelea kuiamini Tanzania na TMA na kuendelea kuisaidia TMA kupitia programu zake mbalimbali za uboreshaji wa huduma za hali ya hewa kikanda na kitaifa ambazo zinatekelezwa kwa ushirikiano na Wadau wa Maendeleo na Nchi Wanachama wa WMO ambapo utekelezaji wake unaendelea vizuri.
“Naendelea kushukuru sana kwa usaidizi wa WMO kupitia programu zake mbalimbali ambazo zinachangia pakubwa katika kuboresha huduma na utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini na nchi nyingine pia kuongeza nguvu katika uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
