Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo, Septemba 9, 2026, amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi.

Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).