……………………………………………………………..
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) inapenda kuutarifu umma kuwa, kufuatia maelekezo ya Serikali kutaka wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, kuanzia siku ya Jumatano tarehe 22 Aprili 2020, wananchi wote watakaotembelea ofisi za Benki Kuu kote nchini watatakiwa kuvaa barakoa (masks) kwa lengo la kujikinga wao wenyewe na kuwakinga wafanyakazi watakaowahudumia dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika kuepuka msongamano, Benki Kuu inawaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla pale inapowezekana, watumie njia mbadala za mawasiliano badala ya kwenda kwenye ofisi za Benki Kuu. Njia hizo ni pamoja na kupiga simu, kutuma barua pepe kupitia [email protected] au [email protected] na pia kutumia nukushi (fax)
namba +255 22 2234217. Aidha, wananchi wanaweza kupata taarifa mbalimbali za Benki Kuu kupitia tovuti yake ya www.bot.go.tz .
Tunatoa wito kwa wananchi wote kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu namna ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono (sanitizers) kila mara na kuepuka msongamano.
Benki Kuu itaendelea kutoa huduma kwa kuzingatia tahadhari zote zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Namba za Simu kwa Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Na. Ofisi ya BOT Namba ya Simu
1. Dar es Salaam (Makao Makuu) +255 22 2234496/7
2. Zanzibar +255 24 2230803
3. Arusha +255 27 254 5541-3/ +25527 254 5482
4. Dodoma +255 26 296 3183/7+255 22 223 2506
5. Mbeya 255 25 250 3321-3
6. Mtwara +255 22 223 2650-1
+255 22 223 2664
7. Mwanza +255 28 250 0313/17
8. Chuo cha BOT Mwanza +255 28 250 0709
+255 28 250 0983