
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akishiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vicent Mpwaji kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam,
iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akimpongeza Askofu Vicent Mpwaji mara baada ya kuwekwa Wakfu kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyofanyika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Vicent Mpwaji, pamoja na wanafamilia wa
Askofu huyo mara baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.

Mhashamu Vicent Mpwaji akiwekwa Wakfu kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyofanyika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 05 Septemba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na wazazi wa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Vicent Mpwaji, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu kwa Askofu huyo, iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.
…….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vincent Mpwaji, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.
Misa hiyo, imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, ambaye ni Askofu kiongozi katika uwekaji Wakfu, akisaidiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Henry Mchamungu.
Pia, Adhimisho hilo limehudhuriwa na Maaskofu kutoka Majimbo Katoliki mbalimbali nchini, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Taasisi, Mapadre, Watawa, familia, ndugu, marafiki pamoja na waumini kutoka maeneo mbalimbali.
