Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania Plc Abednego Mhagama (wa pili kushoto), wakati alipowasili kwenye makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma, kupitia programu ya Vodacom Tanzania Foundation. Madarasa hayo yanalenga kuwapatia wanafunzi na walimu mazingira bora zaidi ya kujifunzia na kufundishia na ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa. Katika awamu hii, shule tatu za msingi za umma katika mikoa ya Pwani, Ruvuma na Morogoro zimenufaika. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Agosti 20, 2026, katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (katikati waliokaa) na Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania, Abednego Mhagama (wa tatu kushoto, waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali mkoani Ruvuma pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Mahilo mkoani humo, kupitia programu ya Vodacom Tanzania Foundation.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (katikati), akipokea maelezo kuhusu madarasa mawili yaliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania Plc katika Shule ya Msingi Mahilo mkoani Ruvuma, yakilenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation za kuimarisha miundombinu ya elimu kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa. Katika awamu hii, shule tatu za msingi za umma katika mikoa ya Pwani, Ruvuma na Morogoro zimenufaika. Hafla ya makabidhiano imefanyika Agosti 20, 2026, katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma. Wengine pichani ni Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa kampuni hiyo, Abednego Mhagama (kushoto) na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald.