Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametangaza kufunguliwa rasmi kwa dirisha la kupokea miswada ya tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kuanzia Agosti 20, 2026.

KAMATI ya Maandalizi ya Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu imefungua milango ya kupokea kazi bunifu kuanzia leo Agosti 19,2026.

Ametoa tangazo hilo leo Agosti 19, 2026 jijini Tanga wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amewataka waandishi bunifu kutuma kazi zao kwaajili ya ushindani kwenye duru la tano la tuzo hizo.

Prof. Mkenda amesema, Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Ubunifu imeingia kwenye orodha ya tuzo bora za uandishi Duniani na kuwataka waandishi wa Tanzania kushiriki kwa wingi ili kuinua lugha ya kiswahili na kupata vitabu vitavyoeleza utamaduni wa Mtanzania kwa undani zaidi.

“Napenda kuwataari kuwa, tuzo hii ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu imeingia kuwa moja ya tuzo bora Duniani, Washindi wa tuzo hii watatangazwa na kupewa zawadi zao Aprili 13, 2027 siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere,” amesema Prof. Mkenda.

Aidha, Prof. Mkenda ameishukuru Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), kwa kuratibu tuzo hii chini ya Kamati ya Maandalizi inayoongozwa na Profesa Penina Mlama kwa mafanikio huku ikiongeza umaarufu ndani na nje ya nchi.

Akielezea mwenendo wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Ubunifu, Prof. Penina Mlama, amesema wanapokea kazi kutoka nyanja nne ambao ni Riwaya, Tamthilia, Ushahiri na Hadithi za Watoto.