Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani
kuhusu operesheni walioiendesha ya kupambana na biashara haramu za
magendo
Sehemu ya waandishi wa habari Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo
JESHI
la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata
ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga ambaye aliyeshirikiana na
wenzake ambao walikimbia wakiwa wameingiza bidhaa za magendo kutoka
nchini India kwa kutumia bandari Bubu ya Kigombe.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda alisema kwamba hatua
ya kukamatwa kwa mkazi huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea
kufanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazibiti biashara za magendo.
Alisema
kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 17 Saa tisa mchana kwenye maeneo ya
Mwarongo Kata ya Marungu Tarafa ya Pongwe ambapo wakiwa kwenye
operesheni hiyo walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa na mifuko 88 ya
sukari yenye kg 50 ambayo imeonekana kutenegenezwa nchini India ikiwa
inaingizwa nchini kwa njia za magendo.
Kamanda huyo alitaja
bidhaa nyengine ambazo zilikamatwa kuwa ni Madumu 45 ya Oili ya Magari
yenye kg 20 kila mmoja na mifuko mitano ya mchele yeye ujazo wa kg 50
kila mmoja ikitokea nchini Pakistani.
Kamanda Chatanda alimtaja
mtuhumiwa ambaye alikamatwa kuwa ni Hassani Tausilo aliyeshirikiana huku
wenzake ambao alikuwa akishirikiana nao kukimbia na kutokomea
kusikojulikana ambao kwa sasa bado wanasakatwa na jeshi hilo kutokana na
kufanya biashara haramu ya magendo
“Sehemu ya sukari ilikamatwa
inasafirishwa kwenye pikipiki tayari ilishashuhwa kwenye Ngalawa na
kwenda kufichwa kwenye mapori yaliyopo kwenye kijiji cha Kigombe na
kuanza kusafrisjwa kwa kutumia pikipiki ambazo pia nazo tulifanikiwa
kuzikamata na mpaka sasa tunazishikia”Alisema kamanda huyo.
Aidha
alisema hivi sasa wanachoendelea nacho ni msako ulioanza kwenye mapori
na kufanikiwa kukamatwa mifuko mengine 78 baada ya mifuko 10 kukamatwa
kwenye pikipiki na mtuhumiw aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo naye
alikimbia huku pia na mafumu 45 na huo mchele.
Hata hivyo
Kamanda huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara watambue kwamba biashara ya
magendo sio biashara tena na itawaingiza kwenye umaskini hivyo waachane
nayo huku akisisitiza kwamba operesheni hiyo ni endelevu na kamwe
haitawapa nafasi na kila anakayejiingia atambua kwamba kwenye biashara
hiyo atambua kwamba atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.