Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga (wa pili kutoka kulia) akisisitiza namna bora ya kutumia adhabu mbadala badala ya vifungo magerezani kwa baadhi ya makosa ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa mahabusu/wafungwa magerezani wakati huu wa kipindi cha ugonjwa wa Corona kwa Wahe. Mahakimu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba , Mhe. Lucia Kairo (katikati)akisisitiza jambo leo kuhusu ufunguaji wa mashauri kwa njia ya mtandao kwa wadau wa Mahakama ili kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama na magerezani kwa upande wa mahabusu na wafungwa ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona .
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na wadau wa Mahakama wakimsikiliza , Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe.Lucia Kairo (hayupo pichani) katika kikao maalumu na wadau wa Mahakama kuangalia namna bora ya kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama, yakiwemo maeneo ya magerezani kwa upande wa mahabusu na wafungwa.
(Picha na Ahmed Mbilinyi – Mahakama Kuu Kanda, Bukoba)