…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Mpwapwa
Serikali imewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto kwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona hasa katika kipindi hiki aambapo wapo nyumbani kutokana na shule kufungwa.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri hivi karibuni wakati akizungumza na Mwandishi wa chombo hiki.
Shekimweri amesema serikali ilishatoa maelekezo hivyo ni jukumu la kila mzazi ama mlezi kuhakikisha mtoto anakuwa salama juu ya janga la corona.
“Serikali ilitoa maelekezo ya kufunga shule kama njia ya kuwaepusha watoto na maambukizi lakini sasa ukipita mtaani tunapishana na watoto jambo ambalo sio zurii kwao,wazazi na walezi zingatieni usalama wa watoto ili kuwaepusha janga hili kwa watoto ” amesisitiza Shekimweri.
Aidha Shekimweri ametoa wito kwa jamii kuacha kufanya mzaha juu ya ugonjwa huo bali kila mmoja afuate maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali ilivyoelekeza.
Shekimweri ameeleza kuwa wazazi na walezi kuwalinda watoto kwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona hasa katika kipindi hichiambacho wapo nyumbani kutokana na shule kufungwa