Na Hellen Mtereko,Mwanza

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inaendelea na utoaji wa elimu kwa wachimbaji wa madini ili wazidi kufahamu namna bora ya utafutaji,uchimbaji na uchenjuaji wa Madini.

Hayo yamebainishwa jana Julai 22, 2026 na Mkurugenzi wa Huduma za Kijiolojia Tanzania (GST) Alex Rutagwelela, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao katika jukwaa la Tano la utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini.

Aidha, amesema kuwa shughuli za kiutafiti katika seta ya madini inafanyila kwa kiwango kikubwa.

Alisema elimu wanayoendelea kuitoa imekuwa chachu kubwa kwa wachimbaji kwani wamekuwa wakifanya shughuli zao kwakufuata utaratibu wa kitaalam ambao umekuwa na tija kubwa katika uzalishaji.

Amesema utafiti unaonesha kuwepo kwa madini katika maeneo mengi hapa nchini hivyo matumizi ya teknolojia nzuri ni muhimu kwa sasa katika uchimbaji na kwenye utafiti wa bidhaa hiyo ili kuwa na uhakika wanapochimba.