Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa SACP Shadrack Masija wakati akizungumza na wananchi wa Korongwe Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika kikao hicho katika kata ya Korongwe.

Na  Neema Mtuka , Nkasi

Wananchi wa Kata ya Korongwe, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameombwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Korongwe ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuimarisha huduma za ulinzi na usalama.

Wito huo umetolewa Julai 19, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, alipokutana na viongozi wa kata, vijiji na vitongoji kujadili kuanza kwa ujenzi wa kituo hicho.

 Amesema mradi huo umetokana na ombi la wananchi ambalo Serikali imelifanyia kazi na tayari fedha za utekelezaji zimetolewa. 

Aidha, amesema ujenzi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kusogeza huduma za ulinzi na usalama karibu na wananchi ili kuimarisha amani na maendeleo.

Kwa niaba ya viongozi wa Kata ya Korongwe, Diwani Mhe. Hamis Huseni ameishukuru Serikali na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kwa kukubali ombi hilo la kamanda wa Polisi mkoa huku akiahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa vifaa vyote vitakavyotumika katika ujenzi wa kituo ambacho, amesema kituo kinajengwa kwa manufaa yao wananchi wa Korongwe.