Wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wametembelea banda la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), wakipata fursa ya kujionea huduma, mifumo ya kisasa ya ugavi wa bidhaa za afya pamoja na nafasi mbalimbali za uwekezaji na ushirikiano zinazotolewa na taasisi hiyo. MSD imeendelea kutumia maonesho hayo kama jukwaa la kuimarisha mahusiano na wadau wa sekta ya afya, huku ikieleza dhamira yake ya kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya wananchi.

WAEKEZAJI WA ALGERIA WATEMBELEA BANDA LA MSD SABASABA
