Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe leo ametembelea banda la Bohari ya Dawa (MSD) katika Maonyesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Saba saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kuwaelekeza MSD kutumia wabunifu wa ndani, ili kuongeza thamani ya mnyororo wa bidhaa za afya nchini.
Dkt. Magembe amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha vijana wabunifu waliojitambulisha na kuidhinishwa ili kuchochea na kukuza ubunifu wa ndani.
“Nitawaletea vijana wabunifu mzungumze nao ili kuona kama wanaweza kupatiwa fursa ya kushirikisha MSD ubunifu wao.” Alisema Dkt.Magembe

