Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa, leo Julai 3, 2026, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya, huku akiitaka kuendelea kutoa huduma kwa weledi na kuwapa kipaumbele wazee wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Akizungumza alipotembelea banda la OTR lililopo katika Ukumbi wa Karume, Dkt. Msemwa alisema ameridhishwa na kazi inayofanywa na taasisi hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuwahudumia wazee kwa heshima na kuwasikiliza kwa makini.
“Pongezi kwa kazi nzuri. Endeleeni kufanya kazi kwa weledi. Wahudumieni vizuri wazee na wasikilizeni, kwani hao ndio wenye nchi,” alisema Dkt. Msemwa.
Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara, maarufu kama Sabasaba, yalianza rasmi Juni 28, 2026, na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13, 2026 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

