Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), akipokelewa na Mkuu wa Mtandao wa Matawi na Mauzo wa Benki ya NMB, Donatus Richard, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Saba Saba. Katika ziara hiyo, Waziri Kapinga alipewa maelezo kuhusu suluhisho mbalimbali za kibenki zinazochochea ukuaji wa biashara, ujumuishaji wa kifedha na mageuzi ya uchumi wa kidijitali nchini.