Maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Ikungi na katika Manispaa ya Singida Juni 27, 2026 ya kusikiliza na kusuluhisha migogoro ya ardhi iliyopo mkoani humo yameanza kutekelezwa leo Juni 30, 2026.

Viongozi na watendaji wa mkoa wa Singida na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakishirikiana na Timu ya Watalaamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walikusanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusuluhisha migogoro ya ardhi ya mamia ya mwananchi waliojitokeza wakiwa na vielelezo mbalimbali.

Akizungumza Mkuuwa wilaya ya Singida alimshukuru Kamishina wa Ardhi, Nathaniel Mathew Nhonge kwa kujitoa kwa moyo kutatua migogoro ya ardhi mkoa wa Singida kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu.

Zoezi hilo limekadiriwa kuendeshwa kwa siku nne ili kuhakikisha kwamba kila mwananchi aliyejitokeza anasikilizwa na suala lake linafanyiwa kazi.

Mkuuwa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, Kamishina wa Ardhi, Nathaniel Mathew Nhonge na Mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Gondwe ni miongoni mwa viongozi walioongoza usuluhishi huo.