Na Mwamvua Mwinyi-Pwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20–25 pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 3–6 yaliyotokea Kitongoji cha Nung’uli, Kijiji cha Kwang’andu, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Chalinze.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Salim Morcase ,alitoa wito kwa mtu yeyote anayewafahamu marehemu au mwenye taarifa zitakazosaidia uchunguzi kujitokeza ili kusaidia kubaini utambulisho wao na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.