Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore akipokea tuzo kutoka kwa Mhe.Prof.Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) baada ya kuibuka mshindi wa Tatu katika kundi la Taasisi zilizofanya vizuri katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2026 katika hafla ya Ufungaji rasmi wa Maadhimisho hayo leo tarehe 23 Juni, 2026 kwenye viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. 

Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Mhe.Ridhiwani Jakaya Kikwete Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tarehe 17 Juni, 2026 na kufungwa tarehe 23 Juni, 2026 na Mhe.Prof.Riziki Shemdoe (Mb) , Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.