Na Atley Kuni, WAF-Arusha

Wataalam wa maabara kutoka taasisi mbalimbali za serikali waliopata mafunzo ya siku tano kuhusu utunzanji wa vimelea na sampuli za muda mrefu, wameaswa kutumia mafunzo hayo na kuwa mabalozi pindi watakapo rejea kwenye vituo vyao. 

Wito huo umetolewa na Bi Valentina Sanga Mratibu wa mradi wa afya moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Juni 19, 2026 wakati akihitimisha mafunzo hayo kwa washiriki 26 kutoka Bara na visiwani.

“Tunatambua kuwa tuna ufinyu wa rasilimali lakini hii haiondoi kutumia rasimali hizo kwa wachache ambao tunaamini pindi warudipo vituoni wanakwenda kuwa chachu ya mabadiliko”, amesema Bi Sanga na kuongeza. 

“Tunaamini mara baada ya mafunzo haya Tanzania sasa inawataalam wa kutunza sampuli kutoka kwenye nyanja zote iwe ni Wanyama, Binadamu au Mazingira yanayo tuzunguka, ninyi ndio Vinara wakwenda kule mabadiliko”, amefafanua Bi. Valentina.

Akizungumza kwa niaba ya Washiriki wengine Mtaalam wa Maabara Edward Shogolo kutoka Central. Tuberculosis Laboratory(CTRL), anaamini walivyokuja ni tofauti na walivyokuja hivyo akaahidi kwenda kutumia maarifa hayo kama nyenzo ya utendaji kazi wao.

Kwa upande wake, Bw. Samwel Mulungu kutoka CIHEB-Tanzania amesema taasisi hiyo kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani (GHS) itaendelea kushirikiana na Serika ili kuhakikisha kile walicho kipanda kwa wataaalam hao kinakuwa na manufaa kwa umma.

“Nimeangalia matokeo ya usaili wetu kabla na baada nimeona kweli kila mmoja wetu alikuwa makini hivyo ujuI huu usiishie kwenye mafunzo haya, hata mkiwa vituoni ukiona jambo hulielewi mpigie mwenzo kumbushaneni”, amesema Mulungu.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu 26 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya, Maabara ya Taifa, hospitali na taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuimarisha usalama wa maabara na ulinzi wa afya ya jamii.