Katika picha ni Waziri wa Ofisi ya Raisi- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kiwete wapili kutoka kulia akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni Tanzu ya VETA ya Ujuzi Mhandisi Marco Kapinga, alipotembelea banda la VETA tarehe 17 Juni, 2026 katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dododma.Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Ofisi ya Raisi- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kiwete, akikabidhiwa zawadi zinazolishwa na Kampuni Tanzu ya VETA ya Ujuzi, leo tarehe 17 Juni, 2026, alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma, Juni 17, 2026.