Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. James Millya akisaini kitabu cha maombolezo ya Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu wa Angola Hayati Manuel Domingos Augusto katika Ubalozi wa Angola jijini Dar es Salaam.
Mhe. Millya amewasilisha salamu za pole kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Lourenço, Balozi wa Angola nchini, Mhe. Balozi Domingos de Almeida da Silva Coelho, wananchi wa Angola pamoja na familia ya Hayati Augusto.
Hayati Augusto alifariki Juni 5, 2026 jijini Luanda akiwa na umri wa miaka 68.
