Na Prisca Libaga RS Arusha
Wanafunzi wa shule za sekondari kutoka Halmashauri zote saba za mkoa wa Arusha wameonyesha vipaji bora katika mbio za riadha kupitia mashindano ya UMISSETA yenye Lengo la kuchuja timu Mkoa itakayoshiriki kwenye mashindano ya ngazi ya taifa yatarajiwa kufanyika June 19, 2026 Mkoani wa Iringa
Mashindano yamefanyika Katika owanja wa sheikh Amir Abeid Jijini Arusha yakihusisha mbio za mita fupi na ndefu, huku washiriki wakionyesha uwezo mkubwa na ushindani wa hali ya juu.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, mratibu wa mashindano Ngoka Kasone amesema mashindano haya yamekuwa chachu ya kuibua vipaji vipya ambavyo vinapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya taifa.
Aidha, mdau wa michezo Silveta Amon amesisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana kuhakikisha vipaji hivi vinapata malezi bora ili kuendeleza tasnia ya michezo nchini.
Naye mwanariadha chipukizi Debora Amos, ambaye ameshiriki katika mashindano ya UMISSETA, amesema anaamini mashindano haya yatamfungulia njia ya kufikia ndoto zake za kimichezo.

