Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo mafunzo elekezi ya awali kwa
watumishi wake mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
Utawala, Samwel Mwashambwa.Mkurugenzi Msaidizi Utawala, Samwel Mwashambwa akimkaribisha mgeni rasmi
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kufunga mafunzo ya awali kwa
watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani).
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine (aliyekaa katikati) mara baada
ya mafunzo hayo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine akifunga
mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wake jijini Dodoma. Wengine kutoka
kushoto ni Afisa Rasilimali Watu, Ahmed Byabato, Mkurugenzi Msaidizi Utawala,
Samwel Mwashambwa wote kutoka Ofisi hiyo na Mkufunzi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Singida, Fadhili Mtinda.
Mkufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Singida, Fadhili
Mtinda akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
**************************
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine amefunga
mafunzo elekezi ya awali (induction course) kwa watumishi wa Ofisi hiyo
mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Katika mafunzo hayo yaliyotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
(TPSC) Tawi la Singida, Balozi Sokoine alisema yatakuwa yamewajenga vizuri
katika kufanya kazi zao.
Alisema kuwa ameridhishwa na mahudhurio ya washriki hao na usikivu
uliooneshwa na watumishi hao na kuwa inadhihirisha namna ambavyo wameiva
kinidhamu.
“Nawapongeza washiriki, naupongeza uongozi wa Chuo cha Utumishi wa Umma
kwa kuandaa mafunzo hayo tunategemea mmepata elimu sahihi na mtafanya
kazi vizuri” alisema Balozi Sokoine.
Kwa upande wake Mkufunzi kutoka TPSC Tawi la Sinigida, Fadhili Mtinda
alisema chuo hicho kimepewa jukumu la kutoa mafunzo, kufanya utafiti na
ushauri wa kitaalamu katika masuala ya Utumishi wa Umma.
Pia Mtinda alitoa shukurani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano kutoka
ngazi ya juu hadi chini ambao imeuonesha kwa siku tatu za mafunzo hayo
ambayoo amehusisha Idara mbalimbali kutoka Ofisi hiyo.