Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na wanafamili, ndugu na jamaa katika swala ya kumswalia marehemu Bi. ARAFA MOH’D SAID ( Maarufu G7 ) aliyeswaliwa katika Masjid LAMIN uliopo KIBWENI na kuzikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi ” B ” Unguja. Inna lilah wainna ilayhi rajiun.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR) Tarehe 31.05.2026.

