******************************
Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) leo tarehe 30 Machi, 2020 amepokea kifaa maalumu cha kunawia mikono kilichotengenezwa na mjasiriamali wa kitanzania ndugu. Jonas Urio (Ambaye anatokea katika mkoa wa Manyara).
Mhe. Bashungwa amempongeza sana ndugu Jonas Urio kwa ubunifu wake huu wa kutengeza kifaa kizuri na bora cha kunawia mikono ambacho kinaweza kutumiwa na
taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuhudumia watu mbalimbali kusafisha mikono yao ili kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Mjasiriamali ndugu Jonas Urio ambaye ni mbunifu wa teknolojia hii ameishukuru Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kumpa ushirikiano tangu awali alipoanza ubunifu wake hadi kufikia hatua hii ambapo ameshasajiliwa na ubunifu wake utambulika.
Ndugu Jonas amesema, “Napokea ushauri wa maboresho ya klifaa hiki niliyopewa na Mhe Waziri na Naibu waziri ambao wote kwa pamoja wamefurahia sana ubunifu wangu, naahidi kufanyia kazi maboresho yote haraka ili kifaa hiki kingie sokoni ili kusaidia wananchi kujisafisha mikono na kupambana na ugonjwa huu wa Corona”