Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewakumbusha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa juu ya umuhimu wa kuishauri Serikali kuhusu ufanisi wa kazi ili kuboresha huduma zinazotolewa na watumishi wa Umma kwa Wananchi.
Mhe. Senyamule amesema hayo Mei 21,2026 Jijini Dodoma, wakati akizindua Baraza jipya la Wafanyakazi katika mkutano uliofanyika Jengo la Mkapa Jijini Dodoma kwa lengo la kufanya uchaguzi wa viongozi wapya baada ya Baraza la awali kumaliza muda wake na kujadili bajeti ya mwaka 2026/2027.
Aidha, amesisitiza wajumbe hao kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledi, maarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu za Utumishi wa Umma.
Kwa upande wake, Afisa Kazi Mfawidhi Mkoa wa Dodoma, Eunice Mmary, amesema Baraza hilo lina jukumu la kujadili na kutathmini utekelezaji wa bajeti pamoja na kutoa ushauri wa kuboresha utendaji kazi na ustawi wa wafanyakazi.
Naye Mjumbe wa Baraza hilo, Mwajabu Nyamkomora, amesema Baraza hilo husaidia kuimarisha mahusiano kati ya viongozi na wafanyakazi pamoja na kutatua changamoto za mahala pa kazi kupitia majadiliano.

