Hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya vyama sita rafiki vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika imefanyika leo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Leadership School. Vyama vinavyoshiriki katika mafunzo hayo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ZANU-PF, African National Congress (ANC), SWAPO, FRELIMO pamoja na MPLA, vikilenga kuendelea kuimarisha mshikamano na misingi ya uongozi wa vyama vya ukombozi barani Afrika.

Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi leo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Stephen Masato Wasira, ambapo yanafanyika kuanzia leo tarehe 18 Mei hadi 25 Mei 2026 kwa lengo la kuwajengea washiriki uwezo wa kiuongozi, usimamizi na kuendeleza tunu za harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.