Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati akiongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi – Ngazi ya Makatibu Wakuu, uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, ambao umejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi hususan hali ya mwenendo wa viashiria vya Uchumi Mpana kwa Nchi zote wanachama wa Jumuiya, ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri.
Na. Joseph Mahumi, WF, Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ameshiriki na kuongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi – Ngazi ya Makatibu Wakuu, uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, ambao umejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi hususan hali ya mwenendo wa viashiria vya Uchumi Mpana kwa Nchi zote wanachama wa Jumuiya, ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elija Mwandumbya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursali Milanzi, na Wataalamu wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Benki Kuu ya Tanzania – BOT, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS.

