*********************
vikuu nchini wametakiwa kuanza kufikiria kujiajiri kwa kuishi na kutumia fursa ya mkopo wa asilimia 4 unaotolewa katika halmashauri kwa vijana ili wawe chachu ya mabadiliko katika jamii kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzao.
Akiongea kwenye Mahafali ya Idara ya vijana wa CCM vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa MNEC UVCCM Mussa Mwakitinya aliemuwakilisha Mwenyekiti wa UVCCM taifa khery James amewataka vijana wasomi hao kuwa sehemu ya mabadiliko na chachu ya maendeleo katika taifa.
Aliwaeleza kuwa mtaani wanahitajika kujipambanua kwa kuanza kutengeneza fursa za ajira na hili wasisubiri watakuwa wameonyesha taswira ya kumsaidia Mh.Rais Dkt.John Magufuli katika Shamira yake kuelekea serikali ya uchumi wa kati wa Viwanda.
“Vijana nendeni mkachangamkie Fursa ya mikopo kuzalisha ajira kwani mnahitaji kulifikiria hili kwa kuanza kujiajiri kwani chama pekee chenye imani ni CCM mkaziishi imani za chama chetu katika jamii kukijenga na kukiimarisha chama kupata ushindi katika chaguzi zilizopo mbele yetu”
Aliwataka vijana hao kucha kujilweza kwa usomi wao bali wakakijenge chama katika jamii kwa misingi ya uwajibikaji na mshikamano utakaosaidia chama hicho kupata ushindi kwa kuwa wakalimani wa shughuli inayofanywa na serikali ya chama chetu.
“Chama chetu kinataka ushindi na Arusha iwe ya kijani vijana jitokezeni kugombea ila nyie mkajipambanue ili tuweze kupata ushindi kwa kuziishi na kutafsiri kanuni na utaratibu wa chama chetu”
Akawaambia vijana hao kufuata Maadili mema wakati watakapopata fursa za ajira kwa kuacha fikra za kupiga na badala yake wawe wazalendo kwa kutanguliza taifa Lao mbele.
Awali Mwenyekiti wa Idara ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha Baraka Solomon amesema kuwa wasomi wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho na nchi kwa ujumla kama watatumia vyema taaluma zao kuikomboa jamii kutoka hapo ilipo kuweza kujiletea maendeleo.
Amesema kuwa mshikamano na ushirikiano uliopo kati yao na viongozi wa chama mkoani hapa ndio umewafikisha hapo katika kukijenga chama ambapo akawataka viongozi kuona umuhimu wa Idara hiyo kuwa na Mali kama ilivyo chama hicho ikiwemo ofisi.
Alisema kuwa vijana wanatakiwa kufanya mambo yao kwa teknolojia na mtandao ndio maana wao kama viongozi walinunua kompyuta na printer kwa ajili ya ofisi na wanampango wa kujenga ofisi ili ziendane na hadhi ya chama hicho.
Kwa upande wake katibu wa mkoa wa Arusha wa chama hicho Mussa Matoroka aliemuwakilisha Mlezi wa chama hicho Humphrey Polepole aliwapongeza Idara hiyo kwa kuhakikisha Arusha inakuwa ya kijani sanjari na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chama hicho na kugombea nafasi za uongozi kwenye chaguzi.
Akawataka kutumia nafasi ya ushirikiano popote watakapoenda kwa kuhubiri amani kwani walifanya uamuzi sahihi kuwa sehemu ya chama hicho nasi tutawapa ushirikiano wakati wowote kukijenga chama chetu ili Arusha iwe ya kijani.
“Serikali inataka kumuweka mtu ambayo habari zake zipo wazi tumieni nafasi hii kuweza kutoa taarifa zenu kwenye kanzidata kwani sasa hamna kushikana mkono bali ujuzi na taarifa zako ndio zitawapata viongozi wenye weledi”
Akaendelea kuwataka kutoa data zao kwa faida ya kujenga mtandao mpana wa uongozi na wasomi hao vijana ndio ambao wataijenga nchi bila kujali uwezo wao akibainisha wa tafakari katika muktadha wa kujiajiri ili kupata suluhu ya tatizo la ajira.
Nae Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa MNEC Annagatha Msuya alisema kuwa mshikamano miongoni mwa vijana hao na kuisemea serikali utasaidia kukijenga chama hicho na kuwataka kuwa mabalozi wazuri na wazalendo huko mitaani kukisemea mazuri yanayofanywa na serikali.